Kamati ya Uchaguzi ya klabu ya Simba imetangaza ratiba ya matukio ya uchaguzi mkuu wa klabu hiyo uliopangwa kufanyika Januari 3, 2027.
Kamati hiyo imetangaza ratiba hiyo kupitia kurasa za mitandao ya kijamii ya Simba.
Tangazo hilo limewekwa hadharani, licha ya Mwenyekiti wa klabu hiyo, Murtaza Mangungu kupinga taratibu zote za uchaguzi huo alipozungumza na waandishi wa habari.

ADVERTISE HERE