Droo ya hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika (CAFCL) imehitimishwa muda mfupi uliopita Simba ikipangwa kundi C.
Katika kundi hilo Simba itapambana na vigogo wengine Orlando Pirates na RS Berkane kuwania tiketi ya robo fainali
Timu nyingine iliyopangwa kundi hilo ni Colombe ya nchini Cameroon ambayo ni mara ya kwanza kushiriki hatua hii.
Simba itakuwa na nafasi ya kumalizana na Pirates ambayo misimu mitatu nyuma walikutana hatua ya robo fainali ya kombe la Shirikisho (CAFCC) na RS Berkane ambao ni msimu mmoja tu uliopita walikutana kwenye fainali ya kombe la Shirikisho.
Haya hapa makundi yote
A - Wiliete SC, Nouadhibou, Petro Atletico, Esperance
B- Cub Africain, MC Alger, Young Africans, Zamalek
C - Colombe, Orlando Prates, Simba, RS Berkane
D - MAS de FES, Horoya AC, Al Hilal, Pyramids