Makundi CAFCL kujulikana leo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
8h ago
Makundi CAFCL kujulikana leo

Macho na masikio ya mashabiki wa soka barani Afrika, hasa nchini Tanzania, leo yatakuwa kwenye Makao Makuu ya Chama cha Soka cha Misri (EFA) jijini Cairo, ambapo Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) litachezesha droo ya hatua ya makundi ya Klabu Bingwa Afrika (CAFCL) na kombe la Shirikisho (CAFCC) msimu wa 2026/27.

Droo hiyo inatarajiwa kuanza rasmi saa 9:00 alasiri kwa saa za Afrika Mashariki (EAT). Habari kubwa na ya mtaji kwa mashabiki wa soka nchini ni kwamba vinara wa ligi kuu ya NBC Simba SC na watani zao Yanga, hawatakutana kwenye hatua hii ya makundi.

Hatua hiyo inakuja baada ya miamba hiyo yote miwili kupangwa kwenye Chungu cha Pili (Pot 2), kutokana na alama zao katika viwango vya ubora wa CAF vya miaka mitano iliyopita.

Sheria za droo ya CAF zinaeleza kuwa timu zilizopo chungu kimoja haziwezi kupangwa kundi moja. Simba SC, waliotinga hatua hii kwa kishindo cha mabao 9-1 kwa jumla dhidi ya 15 de Agosto, wanasubiri kuwafahamu wapinzani wao katika safari ya kusaka taji la Afrika.

Pot 2 inakamilishwa na miamba mingine miwili: Al Hilal (Sudan) na Petro de Luanda (Angola). Hata hivyo, kukwepana kwa Simba na Yanga hakumaanishi kuwa njia itakuwa rahisi.

Kila timu italazimika kukabiliana na mbabe mmoja kutoka Chungu cha Kwanza (Pot 1), ambapo kuna miamba kama Esperance de Tunis (Tunisia), RS Berkane (Morocco), Pyramids FC, na Zamalek SC (Egypt).

Upangaji Kamili wa Vyungu vya Droo ya Leo:

  • Chungu cha 1 (Pot 1): Espérance de Tunis (Tunisia), RS Berkane (Morocco), Pyramids FC (Egypt), Zamalek SC (Egypt).
  • Chungu cha 2 (Pot 2): Simba SC (Tanzania), Young Africans (Tanzania), Al Hilal (Sudan), Petro de Luanda (Angola).
  • Chungu cha 3 (Pot 3): MC Alger (Algeria), Orlando Pirates (South Africa), FC Nouadhibou (Mauritania), Horoya AC (Guinea).
  • Chungu cha 4 (Pot 4): Club Africain (Tunisia), Wiliete SC (Angola), Colombe Sportive (Cameroon), Maghreb de Fes (Morocco).

Droo ya makundi ya msimu huu imekumbwa na mshangao mkubwa baada ya mabingwa watetezi, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, kutupwa nje ya mashindano katika raundi ya awali na timu ngeni ya Wiliete SC kutoka Angola.

Makocha wa timu zote wanasubiri kwa hamu kuona ratiba itakavyoamua hatma zao kuanzia Novemba 2026, huku kukiwa na uwezekano wa kutokea kwa "Kundi la Kifo" (Group of Death).

Kwa mfano, Simba au Yanga zinaweza kuangukia kundi lenye Esperance de Tunis (Pot 1), Orlando Pirates (Pot 3), na Club Africain au Maghreb de Fes (Pot 4) safari ambayo itahitaji misuli na mikakati mizito ya kiufundi.

Droo hii itarushwa mubashara kupitia mifumo ya kidijitali ya CAF ikiwemo chaneli yao ya YouTube ya CAF TV. 

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
3h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
3h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’