Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
9h ago
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba

Klabu ya Simba SC imeingia rasmi kwenye ukurasa mpya wa maboresho ya benchi lake la ufundi baada ya kumtangaza kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Zambia, Honour Janza, kuwa Mkurugenzi mpya wa Ufundi wa klabu hiyo.

Uamuzi huo umetangazwa rasmi na uongozi wa miamba hiyo ya Msimbazi leo, ikiwa ni sehemu ya mikakati ya klabu hiyo kuimarisha mifumo yake ya soka kuanzia timu za vijana hadi timu ya wakubwa.

Janza anakuja na uzoefu mkubwa wa soka la Afrika. Hapa nchini, jina lake si geni kwani amewahi kuhudumu kama Kocha Mkuu wa Namungo FC na baadaye kukabidhiwa mikoba ya kuifundisha timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kwa vipindi tofauti kati ya mwaka 2022 na 2023.

Kimataifa, mafanikio makubwa ya Janza yalikua mwaka 2015 alipoiongoza timu ya taifa ya Zambia (Chipolopolo) kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

Aidha, amewahi kushika wadhifa huo huo wa Mkurugenzi wa Ufundi ndani ya klabu ya ZESCO United ya nchini kwao, hatua inayomfanya kuwa mtu sahihi katika nafasi hiyo mpya ndani ya wekundu wa Msimbazi.

Ujio wa Mzambia huyu unatarajiwa kuongeza tija katika usajili, uratibu wa masuala ya kiufundi na kusimamia falsafa ya soka la Simba. 

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
12h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’