Uongozi wa klabu ya Simba umeanza mazungumzo na kocha mkuu wa timu hiyo Steve Barker kwa ajili ya kumuongezea mkataba wa muda mrefu, imefahamika.
Tangu atue Msimbazi mwezi Disemba 2025, Barker ameifanya Simba kuwa tishio; msimu uliopita akiiongoza kutwaa taji la CRDB.
Aidha msimu huu kocha huyo raia wa Afrika Kusini ameiongoza Simba kushinda mechi zote nane za mwanzo kwenye ligi na kuwaweka Wekundu wa Msimbazi kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama 5 wakiwa na alama 24.
Barker ameweka takwimu za kutisha ndani ya miezi 10 aliyoingoza Simba kwani Wekundu wa Msimbazi hawajapoteza mchezo wowote kwenye ligi tangu achukue mikoba iliyoachwa na Dimitar Pantev.
Inaelezwa Barker alisaini mkataba wa mwaka ambao utamalizika mwishoni mwa Disemba na hivyo Simba sasa ikitaka kumpa mkataba wa mrefu zaidi.
Mpango huo umeharakishwa baada ya kubaini zipo timu zimeanza 'kumyemelea' kocha huyo baada ya kazi nzuri aliyofanya.
Klabu ya Mamelodi Sundowns ni miongoni mwa timu zinazotajwa kuwa mbioni kufanya mabadiliko ya benchi la ufundi baada ya kutupwa nje ya michuano ya ligi ya mabingwa (CAFCL) mapema.
Mamelodi waliondoshwa na Wiliete Sc ya Angola kwa faida ya bado la ugenini baada ya sare ya bao 1-1 nchini Afrika Kusini. Timu hizo zilitoka suluhu ya bila kufungana kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa Angola.