Nitaendelea kuwa Mwanachama hai wa Simba - Try Again

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
11 Sep 2018
Nitaendelea kuwa Mwanachama hai wa Simba - Try Again
Uamuzi wa Kaimu Rais wa Simba Salim Abdallah 'Try Again' wa kutogombea nafasi ya Uwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba kwenye uchaguzi Mkuu utakaofanyika Novemba 03 mwaka huu, umewasononesha wengi.

Try Again ameiongoza Simba kwa mafanikio makubwa tangu alipokaimu nafasi ya aliyekuwa Rais wa klabu hiyo Evans Aveva na Makamu wake Godfrey Nyange Kaburu ambao walishitakiwa Mahakamani kwa kesi ya kuhujumu uchumi.

WanaSimba wengi walitarajia angechukua fomu na hakuna shaka angeweza kushinda kwa kishindo.

Hata hivyo mwenyewe aliamua kutogombea nafasi hiyo kuepusha mgongano wa kimaslahi.

Mwenyewe ameona ni vyema akakaa pembeni hasa baada ya kuiongoza Simba kufanya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji.

Amefafanua kwamba amechukua uamuzi huo ili isije ikatafsiriwa kuwa alikuwa akijitengenezea njia ya kuendelea kubaki madarakani baada ya mafanikio hayo aliyoyapata katika kipindi kifupi cha uongozi wake.

Try Again amesema kutokuwepo kwake kwenye uongozi hakuna maana kuwa hatashirikiana na viongozi watakaochaguliwa.

Amesema ataendelea kubaki akiwa Mwanachama hai wa klabu ya Simba.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
6h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’