Simba yatangaza viingilio vya mchezo wa marudiano dhidi ya 15 de Agosto

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
54m ago
Simba yatangaza viingilio vya mchezo wa marudiano dhidi ya 15 de Agosto

Klabu ya Simba SC imetangaza viingilio vya mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya 15 de Agosto ya Equatorial Guinea, huku ikiwataka mashabiki wake kujitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Uhuru, Oktoba 25, 2026.

Akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo huo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amesema mchezo huo utachezwa Jumapili kuanzia saa 10:00 jioni, akisisitiza umuhimu wa mashabiki kuzingatia muda huo.

“Tumekutana kuzungumzia mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya 15 de Agosto ambao utafanyika Jumapili Oktoba 25, 2026 saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Uhuru. Naomba kusisitiza hapo kwenye muda saa 10 jioni maana mchezo wa jana ulikuwa saa 9 alasiri,” amesema Ahmed Ally.

Viingilio vya mchezo

Ahmed Ally ametangaza viingilio vya mchezo huo kwa madaraja matatu, huku akieleza kuwa tiketi zote zitapatikana kwa njia ya mtandao pekee.

Viingilio vilivyotangazwa ni kama ifuatavyo:

  • Mzunguko: Shilingi 5,000

  • VIP: Shilingi 30,000

  • Platinum: Shilingi 150,000

Kwa mujibu wa Ahmed, mashabiki watanunua tiketi kupitia tovuti rasmi ya mauzo ya tiketi ya klabu, https://simbasc.wanaut.com.

Amesema klabu imeufanyia utafiti mfumo huo na kujiridhisha kuwa utawezesha mashabiki kupata tiketi kwa urahisi bila kulazimika kwenda vituoni.

“Tiketi zote zitauzwa kwa njia ya mtandao. Tumeufanyia utafiti mfumo huu na kujiridhisha utafanya kazi vizuri. Ukiwa na simu ya mkononi ndiyo sehemu ya kununua tiketi,” amesema.

Simba yasukuma matumizi ya teknolojia

Semaji amewataka mashabiki wa Simba kuendana na mabadiliko ya teknolojia kwa kutumia mfumo huo mpya wa ununuzi wa tiketi, akieleza kuwa utarahisisha upatikanaji wa tiketi wakiwa mahali popote.

Amesema utaratibu wa awali uliwafanya mashabiki wengi kusubiri hadi siku ya mwisho kununua tiketi kutokana na usumbufu wa kufika vituoni.

“Dunia imebadilika na sisi Simba Sports Club ni watu wa mwaka wa mbele, lazima twende na mabadiliko ya teknolojia. Sasa ukiwa kazini, ukiwa nyumbani, ukiwa kwenye daladala unaweza kununua tiketi,” amesema Ahmed Ally.

Aidha, amewashauri mashabiki ambao hawana simu janja kuomba msaada kwa rafiki au jirani mwenye simu hiyo ili waweze kununua tiketi na kwenda pamoja uwanjani siku ya mchezo.

Amefafanua kuwa kila mmoja atakuwa na tiketi yake itakayochanganuliwa wakati wa kuingia uwanjani.

Licha ya Simba kuwa na nafasi nzuri ya kusonga mbele kutokana na matokeo ya mchezo wa kwanza, Ahmed Ally amewataka mashabiki kuepuka fikra kwamba mchezo wa marudiano hauna umuhimu tena.

Amesema klabu ina sababu nyingi za kuwataka mashabiki wafike uwanjani, ikiwemo kuwapongeza wachezaji kwa kazi kubwa waliyoifanya na kuwapa heshima wanayostahili.

“Ukiangalia mechi ni kama imeshapoteza mvuto kwa sababu kwa asilimia 80 tuna nafasi ya kwenda makundi, lakini hizo fikra Mwanasimba inabidi kuachana nazo. Tunazo kila sababu za kuipa thamani na heshima mechi hii kwa kwenda uwanjani,” amesema.

Ameongeza kuwa kutohudhuria mchezo huo kunaweza kutafsiriwa kama kutotambua juhudi zilizofanywa na wachezaji wa Simba katika msimu huu.

“Heshima siyo kupost mitandaoni, heshima kwa wachezaji wetu ni kwenda uwanjani. Twendeni tukawapongeze wachezaji wetu. Rai yangu kwa mashabiki wa Simba ni Oktoba 25 isibaki siti hata moja,” amesisitiza.

Simba inalenga kuweka rekodi ya mabao Afrika

Mbali na kuwapongeza wachezaji, Ahmed amesema sababu nyingine ya mashabiki kujitokeza ni kuisukuma timu kuweka rekodi nzuri ya kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Amesema Simba hadi sasa ina mabao sita katika kampeni hiyo ya kufuzu, huku akieleza kuwa klabu inalenga kuongeza idadi ya mabao na kuhakikisha inaweka alama katika mashindano hayo.

“Twendeni tukatengeneze rekodi ya kufuzu Afrika. Ikiwezekana hata kufuzu kwa magoli 16,” amesema Ahmed Ally.

Ameongeza kuwa Uwanja wa Uhuru una uwezo wa kuchukua mashabiki 18,000 pekee, hivyo klabu inahitaji mashabiki kujitokeza kwa wingi ili kuupa mchezo huo hamasa inayostahili.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Doumbia atakuwa bora zaidi - Barker
Doumbia atakuwa bora zaidi - Barker
2h ago
READ MORE β†’
Chilambo labda nafasi ya kipa tu ndio hachezi
Chilambo labda nafasi ya kipa tu ndio hachezi
2h ago
READ MORE β†’
Highlights : 15 de Agosto 1-6 Simba, CAFCL (FT)
Highlights : 15 de Agosto 1-6 Simba, CAFCL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 22 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 22 2026
5h ago
READ MORE β†’
FT : 15 de Agosto 1-6 Simba, CAFCL R1
FT : 15 de Agosto 1-6 Simba, CAFCL R1
19h ago
READ MORE β†’
Kikosi : 15 de Agosto vs Simba, CAFCL R1
Kikosi : 15 de Agosto vs Simba, CAFCL R1
23h ago
READ MORE β†’
BIG SCREEN iko Mwembeyanga
BIG SCREEN iko Mwembeyanga
1d ago
READ MORE β†’
Matchday; 15 de Agosto vs Simba, CAFCL R1
Matchday; 15 de Agosto vs Simba, CAFCL R1
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 21 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 21 2026
1d ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili 15 de Agosto yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili 15 de Agosto yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’