Doumbia atakuwa bora zaidi - Barker

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1h ago
Doumbia atakuwa bora zaidi - Barker

Kocha Mkuu wa Simba SC, Steve Barker, amemwagia sifa kedekede mshambuliaji wake raia wa Mali, Ibrahim Doumbia, kufuatia kiwango safi alichokionyesha kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF CL) huku akisisitiza kuwa mchezaji huyo bado ana nafasi kubwa ya kuwa tishio zaidi kutokana na umri wake mdogo.

Kauli hiyo ya Barker inakuja mara baada ya Doumbia kufungua akaunti yake ya mabao ndani ya kikosi cha Wekundu wa Msimbazi kwa kutupia mabao mawili, katika ushindi mnono wa 6-1 ambao Simba waliupata dhidi ya klabu ya 15 de Agosto.

Kabla ya mchezo huo, Doumbia alikuwa akipitia kipindi kigumu huku akikabiliwa na ukosoaji mkubwa kutoka kwa mashabiki na wachambuzi kutokana na kutoonyesha makali yake ya ufungaji tangu kuanza kwa msimu huu.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya filimbi ya mwisho, Kocha Barker alieleza kuwa mabao hayo yamekuja wakati sahihi wa kumwondolea presha mshambuliaji huyo na kumrejeshea utulivu.

"Nimefurahi sana kwa Doumbia kufunga leo. Washambuliaji wanapokuja kwenye klabu kubwa kama Simba, wanakuwa chini ya presha kubwa sana kutoka kwa mashabiki wanapochelewa kufunga. Mabao haya mawili yanamwondolea mzigo mkubwa kichwani na kumpa ahueni (relief) kubwa," alisema Barker.

Kocha huyo aliongeza kuwa alikuwa na imani kubwa na mchezaji huyo tangu mwanzo kutokana na kile anachokionyesha uwanja wa mazoezi na rekodi yake nzuri aliyotoka nayo nchini Mali, licha ya kuwa shinikizo la mashabiki lilitaka asote benchi.

Barker amewataka mashabiki kuwa wavumilivu akieleza kuwa Doumbia bado ni mchezaji chipukizi mwenye umri wa miaka 22, hivyo bado yuko kwenye mchakato wa kujifunza na kuzoea mifumo ya timu.

"Umri wake unamruhusu, bado ni kijana mdogo sana. Anazidi kukua na kujifunza kila siku. Huu ni mwanzo tu, nina uhakika atakuwa bora zaidi kadri anavyozidi kupata uzoefu hapa nchini na kwenye michuano ya kimataifa," alihitimisha Barker.

Ushindi huo wa mabao 6-1 sio tu kwamba umeisogeza Simba hatua nzuri kueleke makundi, bali pia umerudisha tabasamu kwa Doumbia huku morali kubwa ndani ya kikosi hicho ikionekana kuelekea mechi zao zijazo za Ligi Kuu ya NBC na hatua inayofuata ya CAF.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Chilambo labda nafasi ya kipa tu ndio hachezi
Chilambo labda nafasi ya kipa tu ndio hachezi
1h ago
READ MORE β†’
Highlights : 15 de Agosto 1-6 Simba, CAFCL (FT)
Highlights : 15 de Agosto 1-6 Simba, CAFCL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 22 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 22 2026
4h ago
READ MORE β†’
FT : 15 de Agosto 1-6 Simba, CAFCL R1
FT : 15 de Agosto 1-6 Simba, CAFCL R1
18h ago
READ MORE β†’
Kikosi : 15 de Agosto vs Simba, CAFCL R1
Kikosi : 15 de Agosto vs Simba, CAFCL R1
22h ago
READ MORE β†’
BIG SCREEN iko Mwembeyanga
BIG SCREEN iko Mwembeyanga
1d ago
READ MORE β†’
Matchday; 15 de Agosto vs Simba, CAFCL R1
Matchday; 15 de Agosto vs Simba, CAFCL R1
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 21 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 21 2026
1d ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili 15 de Agosto yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili 15 de Agosto yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
15 de Agosti waruhusu mashabiki
15 de Agosti waruhusu mashabiki
1d ago
READ MORE β†’