Matchday; 15 de Agosto vs Simba, CAFCL R1

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1h ago
Matchday; 15 de Agosto vs Simba, CAFCL R1

Vinara wa Ligi Kuu ya NBC, Simba SC, leo Jumatano wanashuka kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kukabiliana na FC 15 de Agosto ya Guinea ya Ikweta, katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa raundi ya pili ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL).

Mchezo huo unaotarajiwa kuanza majira ya saa 9:00 alasiri, unatarajiwa kuwa na ushindani mkali huku Simba ikipewa nafasi kubwa ya kuondoka na ushindi mnono kutokana na ubora wa kikosi chake na faida ya kucheza nyumbani.

Kikanuni, FC 15 de Agosto ndio wenyeji wa mchezo huu wa leo. Hata hivyo, kutokana na timu hiyo kukosa uwanja wenye vigezo vya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) nchini kwao, walilazimika kuchagua Uwanja wa Uhuru kama uwanja wao wa nyumbani.

Hatua hiyo inaipa Simba faida kubwa ya kimazingira na kisaikolojia dhidi ya wapinzani wao ambao awali waliomba mchezo huo upelekwe Congo.

Mashabiki waruhusiwa uwanjani

Hapo awali kulikuwa na sintofahamu kuhusu uwepo wa mashabiki baada ya wenyeji FC 15 de Agosto kuomba mchezo huo uchezwe bila mashabiki.

Hata hivyo baadae pande zote mbili zikafikia makubaliano katika mazungumzo ya dakika za mwisho, na mashabiki wataruhusiwa kuingia uwanjani kushuhudia mtanange huo.

Mchezo huo uliokuwa uchezwe jana Jumanne ulisogezwa mbele hadi leo baada ya kikosi cha timu hiyo kukwama njiani kutokana na changamoto za usafiri na matatizo ya kifedha, ambapo waliwasili Dar es Salaam jana.

Simba inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na morali ya juu baada ya mfululizo wa ushindi kwenye kila mechi msimu ikiwa ni pamoja na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga SC, kwenye Ligi Kuu ya NBC.

Kwenye hatua ya kwanza ya michuano hii ya CAF, Simba ilionyesha makali makubwa kwa kuiondosha Mighty Wanderers kwa jumla ya mabao 7-1, ikiwemo ushindi wa kishindo wa mabao 6-1 walioupata hapo hapo Uwanja wa Uhuru.

Kocha Mkuu wa Simba Steve Barker amesema leo wanahitaji kushinda mchezo huo na kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kufuzu hatua ya makundi.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 21 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 21 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili 15 de Agosto yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili 15 de Agosto yamekamilika
14h ago
READ MORE β†’
15 de Agosti waruhusu mashabiki
15 de Agosti waruhusu mashabiki
20h ago
READ MORE β†’
15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
23h ago
READ MORE β†’
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
1d ago
READ MORE β†’
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
1d ago
READ MORE β†’
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
1d ago
READ MORE β†’
Huyu Libasse ni moto kweli
Huyu Libasse ni moto kweli
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
1d ago
READ MORE β†’