Kikosi cha Simba kinaendelea na maandalizi yake ya mwisho mwisho kuelekea mchezo wa mkondo wa kwanza kuwania tiketi ya kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya 15 de Agosto.
Jana Simba ilifanya maandalizi yake kwenye viwanja vya Ghymkhana ambapo leo Wekundu wa Msimbazi wanatarajiwa kuhitimisha maandalizi kwenye uwanja wa Uhuru majira ya saa 9 Alasiri.
Kocha Mkuu wa Simba Steve Barker anakiandaa kikosi chake kikamilifu ili kuhakikisha ushindi mnono unapatikana kwenye mchezo huo wa mkondo wa kwanza ili kuwaweka Wekundu wa Msimbazi katika nafasi nzuri ya kutinga hatua ya makundi.










ADVERTISE HERE