Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limefanya mabadiliko ya mwamuzi atakayesimamia mchezo wa mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya FC 15 de Agosto na Simba SC, utakaochezwa Jumatano, Oktoba 21, jijini Dar es Salaam.
Mwamuzi wa kati kutoka Mauritius, Ahmad Imtehaz Heeralall, aliyekuwa amepangwa kuchezesha mchezo huo, ameshindwa kusafiri kwenda Tanzania, hali iliyosababisha CAF kumteua mwamuzi kutoka Misri, Amin Mohamed Omar, kuchukua nafasi yake.
Kwa mujibu wa taarifa, Omar tayari ameondoka Cairo, Misri, na yuko safarini kuelekea Tanzania kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo muhimu wa mashindano ya Afrika.
Mabadiliko hayo yanakuja wakati Simba ikiendelea na maandalizi ya kukabiliana na FC 15 de Agosto katika hatua ya kuwania kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kwa Simba, mchezo huo ni muhimu katika kuweka msingi mzuri kuelekea mechi ya marudiano, huku benchi la ufundi na wachezaji wakitarajiwa kuhakikisha wanatumia vizuri nafasi ya kucheza mbele ya mashabiki wao kwenye mchezo wa pili na kutinga hatua ya makundi