Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
23h ago
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga

Simba SC imepanga kuweka skrini kubwa Mwembeyanga kwa ajili ya mashabiki wake kushuhudia mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC 15 de Agosto, utakaopigwa Jumatano, Oktoba 21, 2026, saa 9:00 alasiri katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Hatua hiyo imekuja baada ya FC 15 de Agosto kukataa mashabiki kuingia uwanjani katika mchezo huo wa kwanza wa raundi ya pili, huku mdhamini mkuu wa Simba, Betway Tanzania, akijitolea kuandaa tukio maalum la kuwakutanisha Wanasimba.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amesema klabu ilijaribu kutumia njia rasmi kushawishi mashabiki waruhusiwe kuingia uwanjani, lakini ombi hilo lilikataliwa.

“Baada ya FC 15 de Agosto kukataa mashabiki, mdhamini wetu mkuu Betway Tanzania akasema, ‘Wanangu, msikae kivyenu, nitafanya jambo kwa ajili ya Simba Sports Club.’ Ametuandalia skrini kubwa ambayo itawekwa hapa Mwembeyanga,” alisema Ahmed.

Kiingilio bure, burudani na zawadi

Ahmed amesema hakutakuwa na kiingilio kwa mashabiki watakaohudhuria Mwembeyanga, huku sharti likiwa ni kuvaa jezi mpya ya Simba ya msimu huu, ambayo amesema bei yake imeshuka hadi Sh 25,000.

Tukio hilo litakuwa na burudani kutoka kwa wasanii King Faida, Msaka Daily na Mczo Morfan, pamoja na DJ Sinyorita na Samio Love. Pia kutakuwa na michezo yenye zawadi, ikiwemo jezi ya Simba iliyosainiwa na Elie Mpanzu.

Kabla ya mchezo wa kimataifa, mashabiki watapata nafasi ya kutazama marudio ya Kariakoo Derby ya Oktoba 10, yakifuatana na uchambuzi. Shughuli zinatarajiwa kuanza saa 4:00 asubuhi.

Simba Isiidharau 15 de Agosto - Ahmed

Licha ya kucheza mchezo wa kwanza nyumbani, Ahmed amesisitiza kuwa Simba haipaswi kuichukulia kirahisi timu hiyo ya Equatorial Guinea, akieleza kuwa wapinzani wao wana kiu kubwa ya kufuzu hatua ya makundi.

“Kinachokupa ushindi si kucheza nyumbani tu, ni maandalizi yako na ubora wako. Niwaambie Wanasimba, twendeni tukaipambanie Simba yetu,” alisema Ahmed.

Ameongeza kuwa malengo ya Simba msimu huu ni makubwa zaidi ya mafanikio ya ndani, akisisitiza kuwa klabu inalenga kufanya vizuri katika mashindano ya Afrika.

Sakuru atoa wito kwa Wanasimba

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Simba, Zubeda Sakuru, amewashukuru mashabiki na mdhamini Betway kwa kuendelea kuiunga mkono klabu, huku akieleza kuwa menejimenti na kikosi vimejiandaa kuelekea mchezo huo.

“Nawaomba kesho kutwa mjitokeze kwa wingi kuja kuangalia mchezo hapa, na tiketi za mchezo wa Jumapili zitauzwa pia hapa,” alisema Zubeda.

Simba inatarajia kucheza mchezo wa marudiano Jumapili, Oktoba 25, 2026, katika Uwanja wa Uhuru, ambapo klabu hiyo inalenga kupata sapoti kubwa ya mashabiki ili kusukuma timu kuelekea hatua ya makundi.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
1h ago
READ MORE β†’
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
5h ago
READ MORE β†’
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
19h ago
READ MORE β†’
Huyu Libasse ni moto kweli
Huyu Libasse ni moto kweli
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
2d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumapili, Oktoba 18 2026
Magazeti ya leo Jumapili, Oktoba 18 2026
2d ago
READ MORE β†’