Barker na kumbukumbu ya kuwakabili 15 de Agosto

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
4d ago
Barker na kumbukumbu ya kuwakabili 15 de Agosto

Jumanne Oktoba 20 Simba itashuka uwanja wa Uhuru kuikabili 15 de Agosto katika mchezo wa mkondo wa kwanza kuwania tiketi ya kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika (CAFCL).

Mtanange huo wa kwanza kati ya mechi mbili za kuamua timu ya kutinga makundi, utapigwa saa 10 jioni.

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Simba kucheza dhidi ya mabingwa hao wa Guinea ya Ikweta lakini kwa kocha Steve Barker haitakuwa mara ya kwanza.

Msimu uliopita Barker wakati anainoa Stellenbosch kabla ya kutua Msimbazi, alikutana na de Agosto kwenye michuano ya kombe la Shirikisho (CAFCC) katika hatua kama hii ya raundi ya pili ya kuwania tiketi ya kutinga makundi.

Mchezo wa kwanza uliopigwa Afrika Kusini Stellenbosch waliibuka na ushindi wa mabao 4-1 huku mechi ya marudiano ugenini mchezo ukimalizika kwa suluhu ya bila kufungana na hivyo Stellenbosch kutinga makundi.

Wakati huu Barker anakutana tena na timu hiyo lakini sasa akiwa na Simba kwenye ligi ya mabingwa huku mechi zote mbili zikipigwa uwanja wa Uhuru.

Barker amesema de Agosto ni timu ambayo taarifa zake sio nyingi hivyo wanapaswa kwenda kuwakabili kwa tahadhari kubwa pamoja na kuwa wana faida ya kucheza mechi zote mbili nyumbani.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
1h ago
READ MORE β†’
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
5h ago
READ MORE β†’
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
19h ago
READ MORE β†’
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
23h ago
READ MORE β†’
Huyu Libasse ni moto kweli
Huyu Libasse ni moto kweli
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
2d ago
READ MORE β†’