De Agosto hawaji kinyonge, sio wa kuwadharau

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
4d ago
De Agosto hawaji kinyonge, sio wa kuwadharau

Kitendo cha klabu ya 15 de Agosto kugomea mashabiki kuingia uwanjani kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza kuwania kufuzu hatua ya makundi ligi ya mabingwa dhidi ya Simba, kinaonyesha timu hiyo ina malengo ya kusaka ushindi na kufuzu hatua ya makundi.

Mechi zote kupigwa uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam ni faida kwa Simba kucheza uwanja wa nyumbani lakini pia de Agosto wangepata mapato na kunufaika kifedha kama wangeruhusu mashabiki kwenye mchezo huo.

Maana yake ni kuwa wamekataa kupata fedha wakiamini mchezo huo kutokuwa na mashabiki unaweza kuwapa nafasi ya kupata matokeo mazuri.

Uamuzi huo umepeleka ujumbe Msimbazi kuwa timu hiyo inakuja kushindana hivyo haipaswi 'kuchukuliwa poa'.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ali amesema wanazichukulia mechi zote mbili kwa uzito sawa lengo likiwa kuhakikisha wanakata tiketi ya hatua ya makundi.

Awali timu hiyo kutoka Guinea ya Ikweta ilitaka mchezo huo uhamishiwe Congo lakini Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) likagomea maombi hayo kwa kuwa muda wa kuruhusu mabadiliko hayo hautoshi.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
1h ago
READ MORE β†’
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
5h ago
READ MORE β†’
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
19h ago
READ MORE β†’
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
23h ago
READ MORE β†’
Huyu Libasse ni moto kweli
Huyu Libasse ni moto kweli
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
2d ago
READ MORE β†’