Klabu ya Simba SC imeweka wazi kuwa malengo yake makuu msimu huu katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) ni kufika hatua ya nusu fainali.
Simba inaamini kuwa uwekezaji na usajili uliofanyika unatosha kuivusha timu hiyo katika hatua zilizowashinda miaka ya nyuma.
Akizungumza kuhusu mikakati ya klabu hiyo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amefichua kuwa uongozi na benchi la ufundi wamejipanga kikamilifu kuhakikisha wanavuka rekodi ya robo fainali waliyoizoea na sasa wanapiga hatua mbele zaidi.
Semaji alibainisha kuwa mabadiliko makubwa yaliyofanyika kwenye kikosi chao, ikiwemo kusajili wachezaji wenye uzoefu mkubwa wa michuano ya kimataifa, ndiyo nguzo kuu inayowapa jeuri ya kuamini kuwa lengo la nusu fainali linawezekana msimu huu.
Meneja huyo aliongeza kuwa maandalizi yote yanaenda vizuri na kikosi kipo kwenye hali nzuri ya kisaikolojia na kimwili kukabiliana na changamoto yoyote mbele yao.
Kipimo cha kwanza cha malengo haya makubwa ya Wekundu wa Msimbazi kitakuwa mnamo Oktoba 20, 2026, ambapo Simba itashuka dimba la Uhuru kumenyana na 15 de Agosto katika mchezo wa kwanza wa raundi ya kwanza.
Mchezo huo utachezwa bila mashabiki, kabla ya timu hizo kurudiana tena mnamo Oktoba 25, 2026 katika uwanja huohuo.