Baada ya Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) kushikilia msimamo wake wa mchezo wa mkondo wa kwanza kuwania kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa kati ya 15 de Agosto dhidi ya Simba kupigwa uwanja wa Uhuru, timu hiyo imegomea mashabiki kuingia kwenye mchezo huo.
15 de Agosto watakuwa wenyeji wa mchezo wa mkondo wa kwanza utakaopigwa Oktoba 20 saa 10 jioni.
Taarifa za uhakika ni kuwa timu hiyo imeweka ngumu mashabiki kuruhusiwa kuingia wakitaka mchezo huo uchezwe bila ya mashabiki.
De Agosto kama wenyeji, wana maamuzi ya mwisho kuhusu suala la mashabiki lakini ni wazi ipo idadi ya mashabiki ambao watapaswa kuruhusu kwa ajili ya timu mgeni ambayo ni Simba.
Simba itakuwa mwenyeji kwenye mchezo wa pili utakaopigwa Oktoba 25 ambao bila shaka dimba la Uhuru litakuwa 'full house'