Klabu ya Simba imethibitisha kuwa mechi zote mbili za kuwania kufuzu hatua ya makundi ligi ya mabingwa dhidi ya 15 de Agosto zitapigwa uwanja wa Uhuru.
Kwa mujibu wa ratiba rasmi iliyotolewa na CAF, mchezo wa mkondo wa kwanza utapigwa Oktoba 20 na mchezo wa marudiano kupigwa Oktoba 25.
Mechi zote zinatarajiwa kupigwa saa 10 jioni.

ADVERTISE HERE