Kagoma amkosha Barker, aipa Simba suluhisho jipya la beki wa kati

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
5d ago
Kagoma amkosha Barker, aipa Simba suluhisho jipya la beki wa kati

Kocha wa Simba, Steve Barker, ameonyesha kuridhishwa na uwezo wa Yusuph Kagoma kucheza nafasi tofauti uwanjani, akifungua uwezekano wa kuendelea kumtumia kiungo huyo kama beki wa kati pale mahitaji ya kikosi yatakapolazimu.

Uamuzi wa Barker kumhamishia Kagoma katika eneo la ulinzi wa kati ulionekana katika ushindi mnono wa mabao 6-1 ambao Simba iliupata dhidi ya Mashujaa ya Kigoma, Jumanne iliyopita, kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo, Kagoma alishirikiana na Ismail Toure kuimarisha ukuta wa ulinzi, akitekeleza jukumu ambalo si la kawaida kwake, kwani amezoeleka zaidi kucheza eneo la kiungo.

Hatua hiyo ilichangiwa na kutokuwepo kwa beki Rushine De Reuck, ambaye kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa anakabiliwa na changamoto za kifamilia. Hata hivyo, Barker aliamua kutumia rasilimali alizonazo ndani ya kikosi badala ya kuruhusu upungufu wa wachezaji kuwa kikwazo.

Barker: Wachezaji wawe tayari kwa majukumu mapya

Barker ameeleza kuwa kuwa na wachezaji wenye uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja ni faida kubwa kwa timu, hasa katika kipindi ambacho kikosi kinaweza kukumbwa na majeraha, kutokuwepo kwa wachezaji au changamoto nyingine zinazoathiri uteuzi.

Kocha huyo amesema amekuwa akiwahimiza wachezaji wake kuwa tayari kukabiliana na majukumu tofauti kulingana na mahitaji ya timu.

“Ni faida kuwa na mchezaji kama Kagoma. Wakati mwingine mnaweza kupoteza wachezaji kutokana na sababu mbalimbali, hivyo ni vizuri. Siku zote nimekuwa nikiwaambia wachezaji kwamba unatakiwa kuwa tayari kwa majukumu tofauti,” alisema Barker.

Kwa upande wake, Kagoma ameonyesha kuwa hana tatizo kupewa jukumu jipya, akibainisha kuwa uzoefu wake wa kucheza nafasi tofauti umemjengea utayari wa kutekeleza maelekezo ya benchi la ufundi.

Kiungo huyo amesema anamudu kucheza kama kiungo mkabaji, kiungo wa kati na hata beki wa kulia, hivyo kuhamishiwa katika eneo la ulinzi wa kati si jambo analolichukulia kama kikwazo.

“Nafasi ambazo nimewahi kucheza, nafikiri hata beki wa kulia nishawahi kucheza, namba sita na namba nane. Maisha kokote,” alisema Kagoma.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
1h ago
READ MORE β†’
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
5h ago
READ MORE β†’
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
19h ago
READ MORE β†’
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
23h ago
READ MORE β†’
Huyu Libasse ni moto kweli
Huyu Libasse ni moto kweli
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
2d ago
READ MORE β†’