Mshambuliaji wa Simba Elie Mpanzu unaweza kusema sasa yuko kwenye kiwango cha maisha yake akiongoza vyema majukumu yake mapya aliyokaidhiwa na kocha Steve Barker.
Katika mechi mbili zilizopita kwenye ligi, Mpanzu amepachika mabao matatu sasa akifikisha mabao manne msimu huu.
Alianza kuwafunga Yanga bao la ushindi lililoihakikishia Simba kuondoka na alama tatu kwa ushindi wa mabao 2-1 na juzi kufunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Mashujaa Fc.
Kiwango bora alichoonyesha katika mechi hizo kimemfanya aondoke na tuzo mbili za nyota wa mchezo.
Ikumukwe ni kocha Barker aliyeamua kumbadilishia majukumu Mpanzu kutoka winga na kuwa mshambuliaji wa kati akianza kumtumia kwenye nafasi hiyo mwishoni mwa msimu uliopita.
Msimu huu Mpanzu ametumika mara nyingi zaidi katika nafasi hiyo baada ya mshambuliaji Ibrahim Doumbia aliyesajiliwa kwenye dirisha lililopita kushindwa kuonyesha makali yake mpaka sasa.