Nguvu sasa ni kwenye ligi ya mabingwa, kufuzu makundi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
5d ago
Nguvu sasa ni kwenye ligi ya mabingwa, kufuzu makundi

Kocha Mkuu wa Simba SC, Steve Barker, amewamwagia sifa wachezaji wake baada ya kugawa dozi ya mabao 6-1 dhidi ya Mashujaa FC, huku akifunguka mikakati mizito ya kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF CL) dhidi ya 15 de Agosto ya Equatorial Guinea.

Ushindi huo mnono uliopatikana jana kwenye Uwanja wa Uhuru unazidi kuikoleza Simba kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC, ikiwa imefanikiwa kudumisha rekodi ya ushindi wa asilimia 100 kwa kukusanya alama 24 katika michezo minane ya kwanza.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo, Barker alisifu morali na makali ya safu yake ya ushambulizi, iliyoongozwa na nyota raia wa DR Congo, Ellie Mpanzu, aliyeng’ara kwa kufunga mabao mawili na kuondoka na tuzo ya mchezaji bora wa mechi kwa mara ya pili mfululizo.

Mabao mengine ya Wekundu wa Msimbazi yalipachikwa wavuni na Libase Gueye, Oura, Abraham Morice, na Ismail Toure.

"Nawapongeza wachezaji kwa kazi kubwa. Walikuwa na kiu ya mabao na walionyesha nidhamu ya hali ya juu tangu dakika ya kwanza hadi ya mwisho. Matokeo haya yanatupa picha halisi ya ubora wa kikosi chetu kuelekea majukumu makubwa yaliyo mbele yetu," alisema Barker.

Ageukia mbio za Kimataifa.

Kocha huyo raia wa Afrika Kusini amesema wanaelekeza nguvu na akili zote kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya pili ya mchujo ya CAF CL dhidi ya 15 de Agosto ambao huenda ukapigwa uwanja wa Uhuru mwishoni mwa wiki.

Kulingana na maelekezo ya CAF, mechi zote mbili dhidi ya 15 de Agosto huenda zikapigwa uwanja wa Uhuru na pengine kuipa Simba nafasi nzuri ya kushinda na kutinga hatua ya makundi.

Barker amebainisha kuwa itakuwa faida ya kipekee ambayo Simba haina budi kuitumia ili kujihakikishia nafasi ya kutinga hatua ya makundi mapema.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
1h ago
READ MORE β†’
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
5h ago
READ MORE β†’
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
19h ago
READ MORE β†’
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
23h ago
READ MORE β†’
Huyu Libasse ni moto kweli
Huyu Libasse ni moto kweli
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
2d ago
READ MORE β†’