FT : Simba 6-1 Mashujaa Fc, NBC PL

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
13 Oct 2026
FT : Simba 6-1 Mashujaa Fc, NBC PL

Wekundu wa Msimbazi Simba SC, wamezidi kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi wakishusha kichapo cha mbwa mwizi kwa Mashujaa FC cha mabao 6-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa leo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Kipigo hicho ni cha pili Simba inatembeza uwanja wa Uhuru baada ya kuibwaga Yanga SC mabao 2-1 kwenye Dabi ya Kariakoo mchezo uliopita, matokeo yanayothibitisha kuwa Wekundu wa Msimbazi kwa sasa wako kwenye kiwango bora zaidi msimu huu chini ya kocha Steve Barker.

Mvua ya mabao ya Simba ilianza mapema dakika ya 16 kupitia kwa winga machachari Libasse Gueye, kabla ya Elie Mpanzu kuongeza goli la pili katika dakika ya 33 na kuipeleka Simba mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 2-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Simba wakionekana kuwa na njaa zaidi ya mabao. Kiungo mshambuliaji Anicet Oura alipachika goli la tatu dakika ya 53, akifuatiwa tena na Elie Mpanzu aliyekamilisha mabao mawili (brace) mnamo dakika ya 58.

Mashujaa FC walijaribu kujinasua kutoka kwenye kamba za Simba na kufanikiwa kupata goli la kufutia machozi dakika ya 64 kupitia kwa mshambuliaji wao Selemani Bwenzi.

Hata hivyo, shangwe hizo za Mashujaa zilidumu kwa muda mfupi kwani kiungo Morice Abraham alizama wavuni dakika ya 61 na beki kisiki Ismael Olivier Toure akahitimisha karamu hiyo ya mabao kwa goli la sita dakika ya 68.

Kwa ushindi huu, Simba SC imejikita thabiti kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC baada ya kufikisha alama 24, ikiwa imeshinda mechi zote nane (8) ilizocheza msimu huu, huku ikionyesha soka safi la kuvutia.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
1h ago
READ MORE β†’
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
5h ago
READ MORE β†’
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
19h ago
READ MORE β†’
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
23h ago
READ MORE β†’
Huyu Libasse ni moto kweli
Huyu Libasse ni moto kweli
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
2d ago
READ MORE β†’