Manara ni wenu hafukuziki - Ahmed Ali awapiga dongo Yanga

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
13 Oct 2026
Manara ni wenu hafukuziki - Ahmed Ali awapiga dongo Yanga

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba SC, Ahmed Ally, amewashukia vikali baadhi ya viongozi na mashabiki wa klabu ya Yanga, kufuatia hatua ya kumshambulia msemaji wa zamani wa klabu hiyo, Haji Manara "Bugatti".

Mzozo huo unakuja baada ya Manara kuonekana kwenye mahojiano ya utani wa soka na Ahmed Ally kufuatia kichapo cha mabao 2-1 ambacho Yanga ilikipata kutoka kwa Simba katika mchezo wa Dabi ya Kariakoo hivi karibuni.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Ahmed Ally amewatolea uvivu Wanayanga akidai kuwa wanatafuta visingizio vya kushindwa kwao kwa kumshambulia mtu ambaye ana historia kubwa na klabu hiyo kuliko wao.

Nyuma Mwiko kuweni wavumilivu

Mlimchukua Mzee Said mkampa Unga wa Ndele akawa kama mjinga, kwenye utambulisho wa Magalasa yenu mkamtumia mshabiki wetu Camera kuhalalisha Mawata Galasa

@hajismanara__ ametembelea kijiwe chake cha Stesheni povu linawatoka,

Sasa tuwaambie Bugati hafukuziki huyo ni Yanga kuliko nyie wote, kama haitoshi nyie mmekuta hapo, ana historia kubwa na klabu hiyo kuliko nyie wakuja

Bugatti ni Yanga for life!!! Huyo ni wenu milele"

Manara ana historia kubwa na soka la Tanzania akiwahi kuzisemea klabu zote mbili Simba na Yanga.

Kwa sasa ni msemaji wa timu zote za Taifa na amekuwa akishiriki matukio mbalimbali ya mijadala ya michezo likiwemo tukio la juzi lililomkutanisha na Semaji

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
1h ago
READ MORE β†’
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
5h ago
READ MORE β†’
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
19h ago
READ MORE β†’
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
23h ago
READ MORE β†’
Huyu Libasse ni moto kweli
Huyu Libasse ni moto kweli
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
2d ago
READ MORE β†’