Ni rasmi klabu ya 15 de Agosto ya Guinea ya Ikweta itatumia uwanja wa Uhuru kama uwanja wake wa nyumbani kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza kuwania tiketi ya kufuzu hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika (CAFCL).
Timu hiyo imelazimika kuleta mchezo huo nchini baada ya kukosa uwanja unaokidhi vigezo vya CAF nchini mwao.
Awali walikuwa na mpango wa kupeleka mchezo Cameroon hata hivyo mpango huo haukufanikiwa kutokana na changamoto zilizotajwa kuwa nje ya uwezo wa klabu hiyo.
15 de Agosto sasa itasafiri kuja Tanzania na kucheza mechi zote mbili dhidi ya Simba katika uwanja wa Uhuru.
ADVERTISE HERE