Kuna uwezekano mkubwa mchezo wa mkondo wa kwanza kuwania tiketi ya kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa kati ya 15 de Agosto ya Guinea ya Ikweta dhidi ya Simba ukapigwa uwanja wa Uhuru.
Taarifa kutoka chanzo cha uhakika zimethibitisha kuwa 15 de Agosto wanalazimika kutafuta uwanja baada ya nchini mwao kukosa uwanja unaokidhi vigezo vya CAF.
Awali timu hiyo ilipanga kupeleka mchezo dhidi ya Simba Cameroon lakini inaelezwa zipo changamoto ambazo zimewafanya washindwe kutekeleza mpango huo.
Timu hiyo imekuwa kwenye mawasiliano na viongozi wa Simba kuona kama wanaweza kucheza mechi zote nchini.
Endapo mpango huo utafanikiwa Wanasimba wanaweza kushuhudia mechi zote mbili zikipigwa dimba la Uhuru.
ADVERTISE HERE