Simba dimbani Jumanne dhidi ya Mashujaa Fc

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
11 Oct 2026
Simba dimbani Jumanne dhidi ya Mashujaa Fc

Baada ya ushindi muhimu wa mabao 2-1 dhidi ya Yanga, kikosi cha Simba hakina muda wa kupoteza kwani Wekundu hao wa Msimbazi keshokutwa Jumanne watakuwa tena uwanjani kucheza mechi nyingine ya ligi.

Kwa mujibu wa ratiba, Simba itashuka uwanja wa Isamuhyo Jumanne Oktoba 13 kuikabili Mashujaa Fc katika mchezo utakaopigwa saa 1 usiku.

Baada ya mchezo huo Wekundu wa Msimbazi watakwea pipa kuelekea Guinea ya Ikweta tayari kwa mchezo wa mkondo wa kwanza kuwania tiketi ya kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa (CAFCL) dhidi ya 15 de Agosto.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Oktoba 17/18 huko Guinea kabla ya Simba kurejea nchini kukamilisha mchezo wa mkondo wa pili

Baada ya ushindi dhidi ya Yanga, Mkufunzi wa Simba Steve Barker aliwapa wachezaji wake nafasi ya kufurahia ushindi huo walioupambania kwa jasho na damu.

Hata hivyo Barker akasisitiza kuwa sherehe hizo zilimalizika jana ileile na leo wanarejea kwenye maandalizi yao kuelekea mchezo unaofuata

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
1h ago
READ MORE β†’
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
5h ago
READ MORE β†’
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
19h ago
READ MORE β†’
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
23h ago
READ MORE β†’
Huyu Libasse ni moto kweli
Huyu Libasse ni moto kweli
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
2d ago
READ MORE β†’