Huyu Barker atengwe, ni masta wa mbinu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
11 Oct 2026
Huyu Barker atengwe, ni masta wa mbinu

Kocha Mkuu wa Simba SC, Steve Barker, amethibitisha kuwa yeye ni fundi wa mbinu (master tactician) kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Yanga SC katika dabi ya kukata na shoka iliyopigwa jana, Oktoba 10, kwenye Uwanja wa Uhuru.

Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa ulimshuhudia Barker akionyesha ukomavu wa hali ya juu wa kimbinu.

Baada ya Yanga kufunga bao mapema, Barker alifanya mabadiliko ya haraka na ya kiufundi yaliyowashangaza wapinzani wao.

Aliwataka wachezaji wake kutopunguza kasi ya kushambulia huku wakiweka kambi kwenye lango la Yanga kwa takribani dakika 30 mpaka kufikia mapumziko.

Kipindi cha pili Barker hakutaka vijana wake wapunguze gia, presha hiyo ililipa dakika ya 67 kwa Neo Maema kusawazisha makosa yake ya kipindi cha kwanza kabla ya Elie Mpanzu kupigilia msumari wa pili. Simba ilitawala mchezo huo kila idara wakiwa na umiliki wa asilia 62 dhidi ya asilimia 38 za wapinzani wao.

Mashuti 14 yalipigwa kwenye lango la Yanga huku sita yakiwa on-target wakati Yanga wakipiga mashuti matatu pekee na moja tu likiwa on target

Ushindi huu unaendeleza rekodi ya kibabe ya kocha huyo raia wa Afrika Kusini dhidi ya watani wao wa jadi. Mpaka sasa, Barker ameshinda mechi mbili za Dabi ya Kariakoo, ikiwemo fainali ya Kombe la Muungano mapema mwaka huu, huku akitoka sare mara mbili na kupoteza mchezo mmoja.

Msimu huu Barker ameingoza Simba kushinda mechi zote saba za mwanzo na kukaa kileleni wakiwa na alama 21. Barker ameshinda jumla ya mechi 17 mfululizo tangu msimu uliopita huku akiwa hajawahi kupoteza mchezo wowote kwenye ligi tangu alipojiunga na Wekundu hao wa Msimbazi mwishoni mwa mwaka 2025

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
1h ago
READ MORE β†’
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
5h ago
READ MORE β†’
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
19h ago
READ MORE β†’
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
23h ago
READ MORE β†’
Huyu Libasse ni moto kweli
Huyu Libasse ni moto kweli
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
2d ago
READ MORE β†’