Rais wa heshima wa klabu ya Simba Bilionea Mohamed Dewji 'Mo' amewapongeza wachezaji, benchi la ufundi na mashabiki kwa ushindi muhimu wa mabao 2-1 dhidi ya Yanga katika mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa uwanja wa Uhuru.
Mabao ya Neo Maema na Elie Mpanzu yameihakikishia Simba ushindi muhimu ambao umewapeleka kileleni mwa msimamo wa ligi wakiendeleza rekodi ya ushindi kwa asilimia 100 msimu huu.
Mo aliweka ahadi ya kutoa Tsh Milioni 500 kama Simba ingeshinda dhidi ya Yanga, hatimaye ahadi hiyo imetimia.
Simba haikushinda tu, bali imewanyanyasa wapinzani wake hao wakuu kwa soka la kitabuni, Steve Barker akituma ujumbe kwa timu nyingine msimu huu Simba 'haicheki na wowote'

ADVERTISE HERE