Ilikuwa ni suala la muda, Simba imeunguruma uwanja wa Uhuru ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Yanga katika mchezo wa ligi kuu ya NBC.
Ni siku ya kipekee kwa mashabiki wa Simba wakishuhudia kandanda safi kutoka kwa timu yao.
Licha ya kuruhusu bao mapema dakika ya tano Yanga wakitangulia kufunga kupitia bao la Peter Shalulile, Simba haikuondoka kwenye mpango wake na kutawala mchezo huo.
Mpaka mapumziko Simba ilionyesha utawala wake ikimiliki mchezo wa asilimia 66 wakiwaweka Yanga nyuma kwa muda mwingi.
Kipindi cha pili ni Simba iliyomiliki mchezo na dakika 67 Neo Maema aliwainua mashabiki wa Simba kwenye viti akiwasawazisha baada ya pasi ya Libasse Gueye.
Wekundu wa Msimbazi waliendelea kuwapelekea moto watani zao ni walihitaji dakika nne tu kuongeza bao la pili kupitia kwa Elie Mpanzu ambaye aliwaramba chenga walinzi wa Yanga pamoja na mlinda lango wao Djigui Diarra kabla ya kuweka mpira kimiani.
Sio ushindi tu kwa Simba lakini furaha zaidi kwa Wanasimba ni kuona timu yao ikicheza kibingwa, hii ndio Simba...!