Matchday : Simba iko kamili, kazi ni moja dhidi ya Yanga leo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
10 Oct 2026
Matchday : Simba iko kamili, kazi ni moja dhidi ya Yanga leo

Wekundu wa Msimbazi, Simba Sc leo watashuka dimba la Uhuru jijini Dar es salaam kuwakabili watani zao Yanga katika mchezo wa ligi kuu ya NBC.

Mtanange huo unatarajiwa kupigwa saa 1 usiku, Simba ikiwa mwenyeji wa mchezo huo.

Ni matokeo ya aina moja tu ambayo Mnyama anahitaji leo, USHINDI ili kupanda kileleni mwa msimamo wa ligi.

Simba ina sababu nyingi za kuhitaji ushindi kwenye mchezo huo lakini kubwa zaidi ni kujiweka katika nafasi nzuri kwenye mbio za kuwania ubingwa msimu huu.

Sifa kuu ya kuwa bingwa kwenye ligi lazima uchukue alama dhidi ya wapinzani wako wakuu. Tayari Mnyama amechukua alama tatu dhidi ya Azam Fc na sasa anazihitaji alama tatu dhidi ya mpinzani wake mkuu Yanga.

Lakini pia leo Simba itashuka uwanja wa Uhuru ikiwa na lengo la kufuta rekodi mbaya ya kukosa ushindi dhidi ya Yanga kwenye mechi za ligi kuu.

Katika misimu minne, Simba imeshinda mchezo mmoja tu dhidi ya Yanga kwenye ligi. Hii ni rekodi mbaya ambayo sasa inapaswa kufika mwisho.

Kwa Simba kuendelea kukosa matokeo mazuri dhidi ya Yanga sio tu inasababisha jambo hilo kuzoeleka, lakini pia ni moja ya sababu iliyopelekea Simba kukosa ubingwa katika kipindi chote ambacho mpinzani wake ametawala.

Mkufunzi wa Simba Steve Barker amesema amekiandaa kikosi chake vyema matarajio yake ni wachezaji kwenda kufanya kile walichokiandaa kwenye uwanja wa mazoezi akiwa na matumaini makubwa ya kuibuka na ushindi.

Barker alikiri mchezo hautakuwa mwepesi kwa sababu wapinzani wao Yanga nao wana ubora katika baadhi ya maeneo hivyo watawakabili kwa kuzingatia mpango waliouandaa huku wakitumia madhaifu yao kuwaadhibu.

Mtanange huo unatarajiwa kupigwa kuanzia saa 1 usiku.

Kila la kheri Simba, kila la kheri Mnyama.. Kila la kheri Wekundu wa Msimbazi...!

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
1h ago
READ MORE β†’
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
5h ago
READ MORE β†’
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
19h ago
READ MORE β†’
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
23h ago
READ MORE β†’
Huyu Libasse ni moto kweli
Huyu Libasse ni moto kweli
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
2d ago
READ MORE β†’