Bodi ya ligi yahakikisha usalama vyumba vya kubadilishia nguo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
10 Oct 2026
Bodi ya ligi yahakikisha usalama vyumba vya kubadilishia nguo

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeimarisha hatua za kuhakikisha usalama wa vyumba vya kubadilishia nguo za wachezaji kwa kusisitiza matumizi ya vifaa maalumu vya kupima ubora wa hewa vinavyojulikana kama Gas Detectors wakati wa mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kupitia taarifa yake kwa umma iliyotolewa Oktoba 9, 2026, TPLB imeeleza kuwa vifaa hivyo vitatumika kukagua vyumba vya kubadilishia nguo ili kuhakikisha mazingira yanakuwa salama kwa wachezaji, benchi la ufundi na maafisa wa timu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ukaguzi utaanza mara baada ya vyumba vya kubadilishia nguo kukabidhiwa kwa timu husika na utaendelea hadi mchezo utakapokamilika. Lengo ni kubaini uwepo wa gesi au hali isiyo ya kawaida ya hewa inayoweza kuhatarisha afya na usalama wa watumiaji wa vyumba hivyo.

Vifaa hivyo vimeanza kutumika

TPLB imesema matumizi ya vifaa hivyo yalianza Oktoba 8, 2026, ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa kiusalama unaotekelezwa katika viwanja vyote nchini vinavyotumika kwa michezo ya ligi.

Hatua hiyo inalenga kuhakikisha vyumba vya kubadilishia nguo vinakuwa na mazingira yanayofaa kwa matumizi ya timu kabla, wakati na baada ya michezo, huku afya na usalama wa wachezaji vikipewa kipaumbele.

Bodi hiyo imesisitiza kuwa itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa soka nchini kuhakikisha mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara zinafanyika katika mazingira salama, kwa kuzingatia taratibu na viwango vya usalama vinavyotakiwa.

Utekelezaji wa utaratibu huo ni sehemu ya juhudi za kuimarisha usimamizi wa usalama viwanjani na kulinda afya za wachezaji, benchi la ufundi pamoja na maafisa wengine wa timu.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
1h ago
READ MORE β†’
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
5h ago
READ MORE β†’
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
19h ago
READ MORE β†’
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
23h ago
READ MORE β†’
Huyu Libasse ni moto kweli
Huyu Libasse ni moto kweli
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
2d ago
READ MORE β†’