Kocha Mkuu wa Simba Steve Barker amesema maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Yanga yamekamilika huku kikosi chake kikiwa na matarajio makubwa ya kushinda mchezo huo.
Akizungumza kwenye mkutano na wanahabari kuelekea mchezo huo mapema leo, Barker amesema wanatambua ugumu na ukubwa wa mchezo huo lakini anaamini kwenye mipango na maandalizi yao kuelekea mchezo huo.
"Maandalizi kwa upande wetu yamekwenda vizuri, tunatambua hautakuwa mchezo rahisi kama ilivyo ukubwa wa mechi yenyewe."
"Ila tumejiandaa vyema, tumefanya kazi kubwa kwenye uwanja wa mazoezi, morali ya wachezaji iko juu."
"Naamini tutakuwa na mechi nzuri na kupata ushindi," alisema Barker.
Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, kiungo Neo Maema amesema wachezaji wako tayari wakiwa na ari kubwa kuelekea mchezo huo.
Amesema wanatambua ugumu wa mchezo huo lakini wameweka malengo na watahakikisha wanaibuka na ushindi.
"Wchezaji kwa upande wetu tuna morali nzuri na kubwa, tunafahamu tunakwenda kucheza mechi ngumu na muhimu sana kwetu"
"Tumejiwekea malengo na tunahitaji kwenda kuyatimiza. Tupo tayari kupambana na kupata matokeo mazuri kwenye mchezo huo," alisema Maema
""