Mwamuzi Ahmed Arajiga anatarajiwa kuwa katikati ya vita ya heshima na pointi tatu wakati Simba na Yanga zitakapokutana katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC utakaopigwa Jumamosi, Oktoba 10, kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Baada ya kuziamua timu hizo kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii August 12, Arajiga amepewa tena dhamana ya kusimamia pambano hilo kubwa linalokutanisha watani wa jadi wa soka la Tanzania.
Waamuzi watakaoshirikiana naye ni:
-
Mohamed Mkono β Mwamuzi msaidizi namba moja.
-
Ally Ramadhani β Mwamuzi msaidizi namba mbili.
Mchezo huo wa Ligi Kuu ya NBC utapigwa Jumamosi, Oktoba 10, katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, kuanzia saa 1:00 usiku.

ADVERTISE HERE