Baada ya kukosekana kikosini tangu mwanzoni mwa msimu huu, nahodha wa Simba Shomari Kapombe amerejea kikosini akiwa sehemu ya kikosi kinachokamilisha maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Yanga utakaopigwa kesho Jumamosi kwenye uwanja wa Uhuru.
Kapombe aliumia mkono nchini Rwanda wakati Simba ikishiriki michuano ya CECAFA Kagame Cup ikiwa sehemu ya maandalizi kuelekea msimu huu.
Urejeo wake ni habari njema kwa benchi la ufundi kwani anatarajiwa kuongeza machaguo ya wachezaji kwenye safu ya ulinzi upande wa kulia.



ADVERTISE HERE