Kaimu Rais wa Simba Salim Abdallah 'Try Again' amethibitisha kuwa hatagombea nafasi hiyo anayoikaimu.
Leo ikiwa siku ya mwisho kwa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi kwenye klabu ya Simba kuchukua fomu, Salim amesema baada ya kuiongoza timu hiyo kwa mafanikio tangu msimu uliopita, ameona ni vyema akawaachia wengine waendeleze gurudumu.
Salim pia amesema kwa kuwa yeye ameshiriki kikamilifu katika mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uongozi wa klabu ya Simba, atasababisha mgongano wa kimaslahi kama atagombea nafasi hiyo.
Wakati zoezi la kuchukua fomu likifikia tamati leo, mpaka jana hakukuwa na Mwanachama aliyejitokeza kuchukua fomu kugombea nafasi ya Mwenyekiti.

ADVERTISE HERE