Klabu ya Simba imethibitisha mchezo wa ligi kuu dhidi ya Yanga utapigwa Jumamosi, Oktoba 10 kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Simba ndio wenyeji wa mchezo huo ambao utapigwa kuanzia saa 1 usiku.
Baada ya majadiliano ya wiki kadhaa, hatimaye mchezo huo unarudi uwanja wa Uhuru 'Shamba la Bibi' baada ya muda mrefu kupita.
Uwanja wa Uhuru umefanyiwa maboresho na sasa uko tayari kwa mchezo huo mkubwa wenye hadhi ya Kimataifa.
ADVERTISE HERE