Barker aweka mkakati wa ushindi Kariakoo Derby

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
8 Oct 2026
Barker aweka mkakati wa ushindi Kariakoo Derby

Baada ya kurejea jijini Dar es Salaam kutoka Afrika Kusini ambako waliweka kambi ya siku 10, kikosi cha Simba leo kinatarajiwa kuingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kuelekea Kariakoo Derby dhidi ya Yanga, mchezo unaotarajiwa kuchezwa Jumamosi, Oktoba 10.

Kambi hiyo ya Afrika Kusini ilikuwa sehemu muhimu ya maandalizi ya Simba kuelekea mchezo huo mkubwa, huku benchi la ufundi likitumia muda huo kuendelea kujenga utayari wa kimwili, kiufundi na kiakili wa wachezaji.

Kuelekea dabi hiyo yenye mvuto mkubwa nchini, kocha mkuu wa Simba, Steve Barker, ameweka wazi maeneo ambayo anaamini yanaweza kuwa na umuhimu mkubwa katika kutengeneza matokeo, akisisitiza uimara wa timu bila mpira, utulivu katika kumiliki mpira pamoja na matumizi sahihi ya nafasi.

Barker amesisitiza kuwa Kariakoo Derby si mchezo wa kuingia uwanjani kwa pupa, bali ni mechi inayohitaji nidhamu ya hali ya juu na umakini katika kila hatua, kutokana na presha na ushindani unaoambatana na pambano hilo.

Barker aweka mkazo kwenye uimara bila mpira

Jambo la kwanza ambalo kocha huyo ameliweka mbele ni namna Simba itakavyokuwa imara inapokuwa haina mpira.

Barker amesema katika mchezo mkubwa kama Kariakoo Derby, timu inaweza kuadhibiwa haraka kutokana na kosa dogo, hivyo amewataka wachezaji wake kuwa makini katika namna wanavyolinda nafasi zao na kuzuia Yanga kupata maeneo ya kutengeneza mashambulizi.

“Tunapaswa kuwa makini zaidi tunapokuwa hatuna mpira, nisingependa kuona makosa rahisi ambayo yanaweza kutugharimu kwa sababu katika mchezo mkubwa kama huu, wakati mwingine kosa moja linaweza kuamua matokeo,” amesema Barker.

Utulivu na umiliki wa mpira

Eneo jingine ambalo Barker ameliweka kwenye mpango wake ni suala la utulivu na umiliki wa mpira.

Kocha huyo anataka Simba icheze kwa kujiamini hata inapokabiliwa na presha, akisisitiza kuwa wachezaji hawapaswi kufanya maamuzi ya haraka kwa sababu ya presha ya mchezo.

Badala yake, anataka timu yake itumie umiliki wa mpira kama silaha ya kuidhibiti mechi, kupunguza kasi ya mpinzani na kutengeneza nafasi kwa wakati unaofaa.

Kwa mtazamo huo, Simba itahitaji utulivu katika kujenga mashambulizi kutoka nyuma, huku wachezaji wa kati wakipewa jukumu muhimu la kuhakikisha timu haipotezi mpira kirahisi na inabaki na udhibiti wa mchezo.

Nafasi chache, lazima Zitumiwe

Barker pia amegusa eneo ambalo linaweza kuwa na umuhimu mkubwa katika kuamua matokeo ya dabi hiyo, matumizi ya nafasi.

Kocha huyo anataka washambuliaji wake kuwa na umakini zaidi wanapofika katika eneo la mwisho la uwanja, akitambua kuwa michezo ya aina hii mara nyingi haitoi nafasi nyingi za wazi.

“Tunajua hatutapata nafasi nyingi katika mchezo huu, tunapopata nafasi lazima tuwe na ubora wa kutosha kuzitumia. Hilo ni jambo ambalo tumekuwa tukilifanyia kazi mara kwa mara,” alisema.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
1h ago
READ MORE β†’
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
5h ago
READ MORE β†’
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
19h ago
READ MORE β†’
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
23h ago
READ MORE β†’
Huyu Libasse ni moto kweli
Huyu Libasse ni moto kweli
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
2d ago
READ MORE β†’