Wachezaji wanaitaka Kariakoo Derby Jumamosi - Ahmed

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
6 Oct 2026
Wachezaji wanaitaka Kariakoo Derby Jumamosi - Ahmed

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ali amewahakikishia mashabiki wa timu hiyo kuwa wamejipanga vyema kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Yanga utakaopigwa Jumamosi, Oktoba 10 kwenye uwanja wa Uhuru.

Ahmed amesema baada ya kikosi kurejea nchini wakitoka Afrika Kusini ambako walikamilisha kambi ya siku 10, timu inatarajiwa kurejea mazoezini leo wakiingia kambini moja kwa moja kukamilisha maandalizi ya mchezo huo.

Ahmed amesema wachezaji wana ari na morali kubwa kila mmoja akiwa na shauku kubwa ya mchezo huo

"Wachezaji wanautazama mchezo huu kwa jisho la matamanio makubwa, kitendo cha kuwapeleka nje ya nchi kuweka kambi huo ni ujumbe kuonyesha kwa kiasi gani tumedhamiria kufanya vizuri kwenye mchezo huu pamoja na mechi nyingine zinazokuja"

"Morali ya wachezaji iko juu, ligi tumeanza vizuri bila kupoteza wala sare hivyo tunataka kuendeleza mwenendo huo kwa kupata ushindi kwenye kila mechi."

"Simba dhidi ya Yanga ni mechi ya kimaamuzi, hii ni mechi ambayo unakwenda kupata ubora halisi wa timu yako. Kipimo cha usajili na maandalizi tuliyofanya ni katika mchezo huu Jumamosi Oktoba 10"

"Mashabiki wa Simba waje uwanjani kwa wingi, maandalizi yamekwenda vizuri na kila kitu kiko sawa," alisema Ahmed.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
1h ago
READ MORE β†’
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
5h ago
READ MORE β†’
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
19h ago
READ MORE β†’
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
23h ago
READ MORE β†’
Huyu Libasse ni moto kweli
Huyu Libasse ni moto kweli
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
2d ago
READ MORE β†’