Hatutaingia kinyonge Kariakoo Derby - Rweyemamu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
5 Oct 2026
Hatutaingia kinyonge Kariakoo Derby - Rweyemamu

Meneja wa Simba SC, Patrick Rweyemamu, ametuma salamu za onyo kwa watani wao wa jadi, Yanga SC, akisisitiza kuwa kikosi chao hakitaingia kinyonge katika mchezo ujao wa Dabi ya Kariakoo utakaopigwa Jumamosi, Oktoba 10, 2026.

Kauli hiyo ya Rweyemamu imekuja mara baada ya kikosi cha Simba kuwasili jijini Dar es Salaam jana kikitokea nchini Afrika Kusini, ambako kilikuwa kimeweka kambi maalum ya siku 10 kujiandaa na mchezo huo wa kukata na shoka pamoja na mashindano mengine ya msimu huu.

Akizungumza na waandishi wa habari, Rweyemamu alikiri kuwa Yanga wamekuwa na matokeo mazuri dhidi yao katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, lakini akaweka wazi kuwa historia hiyo haitabebwa kwenye mchezo ujao.

"Hatutaingia kinyonge kabisa, na utakuwa mchezo wa kufa na kupona. Tunafahamu rekodi zao dhidi yetu kwa siku za nyuma, lakini safari hii tumejipanga na wasitegemee kupata matokeo kwa urahisi," alisema Rweyemamu.

Kuhusu kambi yao ya Afrika Kusini, Meneja huyo alieleza kuwa imewasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza utulivu na utimamu wa mwili kwa wachezaji.

Licha ya Simba kupoteza mechi zote mbili za kirafiki walizocheza nchini humo, wakikubali kipigo cha 1-0 kutoka kwa Polokwane City na 2-1 dhidi ya Sekhukhune United, Rweyemamu alifafanua kuwa matokeo hayo hayawapi wasiwasi kwani benchi la ufundi lilikuwa likiangalia makosa na mifumo.

Meneja huyo alihitimisha kwa kutoa wito kwa mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi uwanjani siku ya Jumamosi ili kuipa timu sapoti ya hali ya juu, huku akiahidi kuwa wachezaji wako tayari kupambana hadi tone la mwisho la jasho ili kurudisha heshima ya klabu hiyo.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
1h ago
READ MORE β†’
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
5h ago
READ MORE β†’
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
19h ago
READ MORE β†’
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
23h ago
READ MORE β†’
Huyu Libasse ni moto kweli
Huyu Libasse ni moto kweli
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
2d ago
READ MORE β†’