Simba Marathon yafana Dar

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
4 Oct 2026
Simba Marathon yafana Dar

Jiji la Dar es Salaam leo limesimama kwa masaa kadhaa kufuatia kufanyika kwa tamasha la kihistoria la mbio za Simba Marathon, ambalo limeacha gumzo katika fukwe za Coco Beach na maeneo ya jirani.

Mbio hizo zilizofanyika kwa mara ya kwanza kabisa nchini, zimebeba sura ya kipekee huku zikivuta maelfu ya washiriki, wapenzi wa michezo, na mashabiki wa klabu ya Simba waliofurika tangu alfajiri ya leo kushuhudia na kushiriki tukio hilo la kihistoria.

Simbu amwaga hamasa

Kivutio kikubwa katika mbio hizo kilikuwa ni uwepo wa mwanariadha nguli wa kimataifa wa Tanzania, Felix Simbu, aliyeshiriki kama miongoni mwa wageni mashuhuri.

Uwepo wa Simbu uliongeza hadhi ya mashindano hayo na kuwapa hamasa kubwa wakimbiaji chipukizi na mashabiki waliopata fursa ya kukimbia naye bega kwa bega kwenye vitengo vya mizunguko ya kilomita 5, 10, na nusu marathon (kilomita 21).

Mbali na ushindani wa medali na zawadi, Simba Marathon imegusa mioyo ya wengi kutokana na lengo lake kuu la kijamii. Sehemu kubwa ya mapato yaliyokusanywa kupitia usajili wa mbio hizo inakwenda moja kwa moja kufadhili matibabu na kutoa bima za afya kwa wachezaji wa zamani wa Simba SC wenye uhitaji, kuanzia wale walioichezea klabu hiyo tangu mwaka 1936 hadi sasa.

Hatua hiyo imepongezwa na wadau wengi wa soka nchini wakieleza kuwa ni utaratibu wa kiungwana katika kuwajali mashujaa waliotengeneza historia ya klabu hiyo kongwe.

Mbio hizi zimekuwa sehemu ya shamrashamra kubwa ya kuadhimisha miaka 90 tangu kuanzishwa kwake. Viongozi wa Simba wameeleza kuridhishwa kwao na muitikio wa mashabiki waliojitokeza kufikia lengo la washiriki takriban 5,000, huku wakiahidi kuwa mafanikio ya leo yanatoa dira mpya ya michezo.

Kufuatia mafanikio hayo makubwa yaliyoshuhudiwa leo fukweni Coco Beach, uongozi wa klabu hiyo umetangaza rasmi kuwa kuanzia mwaka 2027, Simba Marathon itakuwa endelevu. Mbio hizo zitaingizwa rasmi kwenye kalenda ya matukio ya kila mwaka ya klabu hiyo na kuwa sehemu ya tamasha maarufu la Simba DAY.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
1h ago
READ MORE β†’
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
5h ago
READ MORE β†’
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
19h ago
READ MORE β†’
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
23h ago
READ MORE β†’
Huyu Libasse ni moto kweli
Huyu Libasse ni moto kweli
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
2d ago
READ MORE β†’