Keletso afichua alivyoitosa Kaizer Chiefs na kutua Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
3 Oct 2026
Keletso afichua alivyoitosa Kaizer Chiefs na kutua Simba

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba SC, Keletso Makgalwa, amefichua sababu zilizomfanya kuzitosa ofa za miamba ya soka ya Afrika Kusini, Kaizer Chiefs na kuamua kutua Msimbazi.

Makgalwa, ambaye alitua kwa Wekundu wa Msimbazi akitokea Sekhukhune United ya nchini kwao Afrika Kusini, amefunguka kuwa maamuzi yake yalitokana na mipango thabiti ya viongozi wa Simba pamoja na kiu yake ya kutafuta changamoto mpya nje ya ardhi ya nyumbani.

Akizungumza kwenye mahojiano na wanahabari Afrika Kusini ikuhusu dili lake na Kaizer Chiefs lilivyokwama, nyota huyo amekiri kuwa klabu hiyo maarufu kama 'Amakhosi' ilionyesha nia kubwa ya kumsajili na hata kumpa ofa nzuri ya kifedha, lakini walikosa kasi katika kufanya maamuzi.

"Moyo wangu ulikuwa umeshamaliza safari ya kucheza Afrika Kusini, nilitaka kwenda nje. Kaizer Chiefs walikuja na ofa nzuri sana, lakini wakati wao wanasuasua na kujipanga, viongozi wa Simba walikuja kwa kasi na kuonyesha nia ya dhati ya kunihitaji. Sikutaka kusubiri, nikasaini Simba," alisema Makgalwa.

Licha ya kuwapiga chini Kaizer Chiefs kwa sasa, Makgalwa ameweka wazi kuwa kuichezea klabu hiyo ya Soweto ilikuwa ni ndoto yake ya tangu utotoni akiwa anakuwa huko Mokopane, na haifungi milango ya kurejea huko hapo baadaye maji yakirudi mtoni.

"Kucheza Chiefs ni ndoto ya kila mtoto wa Afrika Kusini. Kwa sasa niko Simba, lakini sijaifunga milango hiyo kabisa. Lolote linaweza kutokea huko mbeleni," aliongeza.

Akizungumzia kuhusishwa kwake na Yanga, kiungo mshambuliaji huyo alidokeza kuwa kulikuwa na mazungumzo na ofa mezani, lakini wepesi na ushawishi wa mradi wa Simba ndivyo vilivyomvutia zaidi kuchagua upande mwekundu wa Msimbazi.

Mchezaji huyo amewatoa hofu mashabiki wa Simba akiahidi kupambana kufa na pona ili kuisaidia timu hiyo kurudisha heshima yake. Makgalwa amebainisha kuwa malengo yake makuu msimu huu ni kuhakikisha anakuwa msaada kwa Simba iliyoweka mkakati wa kutwaa mataji ya ndani pamoja na kufanya vizuri katika anga la kimataifa

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
1h ago
READ MORE β†’
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
5h ago
READ MORE β†’
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
19h ago
READ MORE β†’
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
23h ago
READ MORE β†’
Huyu Libasse ni moto kweli
Huyu Libasse ni moto kweli
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
2d ago
READ MORE β†’