Simba Marathon yazidi kunoga

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
2 Oct 2026
Simba Marathon yazidi kunoga

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi klabu ya Simba Sc, Crescentius Magori pamoja na wajumbe wa Bodi, CPA Issa Masoud, Selemani Haroub na Mtendaji Mkuu wa Simba Zubeda Sakuru wamethibitisha ushiriki wao Simba Marathon Oktoba 04 2026.

Mabosi hao wa Simba tayari wamechukua vifaa vyao kushiriki wakiungana na mamia ya Wanasimba ambao wamejiandikisha kushiriki tukio hilo la kihistoria ambalo linakwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 90 ya klabu ya Simba.

Jana Mwanariadha nyota wa Tanzania, Alphonce Simbu, alithibitisha atakuwa miongoni mwa washiriki wakubwa katika Simba Marathon 2026, itakayofanyika Jumapili, Oktoba 4, 2026, katika Ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam.

Ushiriki wa Simbu, ambaye ni mmoja wa wanariadha mashuhuri nchini na mwenye uzoefu wa mashindano makubwa ya kimataifa, umeongeza mvuto katika mbio hizo zinazoandaliwa na Simba Sports Club ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 90 ya klabu hiyo.

Simba Marathon ya mwaka huu itakuwa na mbio za umbali wa kilomita 5, 10 na 21, hivyo kuwapa nafasi washiriki wenye viwango tofauti vya uwezo kushiriki katika tukio hilo.

Simbu amewahi kuiwakilisha Tanzania katika mashindano makubwa ya kimataifa, ikiwemo Boston Marathon na Michezo ya Olimpiki, jambo linalofanya uwepo wake katika mbio hizo kuwa kivutio kwa wanariadha chipukizi na mashabiki wa riadha.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
1h ago
READ MORE β†’
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
5h ago
READ MORE β†’
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
19h ago
READ MORE β†’
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
23h ago
READ MORE β†’
Huyu Libasse ni moto kweli
Huyu Libasse ni moto kweli
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
2d ago
READ MORE β†’