Oktoba haina kupoa kwa Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
2 Oct 2026
Oktoba haina kupoa kwa Simba

Kikosi cha Simba kinaendelea na maandalizi yake Afrika Kusini kuanza kampeni ya kukusanya alama tatu kwenye kila mchezo katika mwezi huu wa Oktoba 2026.

Miamba hiyo ya Msimbazi, chini ya Kocha Mkuu Steve Barker, inakabiliwa na mfululizo wa mechi za ndani na kimataifa zitakazoweka jaribio kubwa kwa wachezaji kutokana na ukaribu wake.

Kwa sasa, kikosi cha Wekundu wa Msimbazi kimejichimbia nchini Afrika Kusini kwa kambi maalum ya siku 10. Wakiwa huko, Simba wanapima mitambo yao kupitia mechi mbili za kirafiki dhidi ya Polokwane City na Sekhukhune United kabla ya kurejea nchini tayari kwa dabi ya Kariakoo.

Shughuli itaanza Oktoba 10, ambapo Wekundu hao wa Msimbazi watakuwa wenyeji wa watani wao wa jadi, Yanga, katika Dabi ya Kariakoo itakayopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Siku tatu baada ya dabi hiyo, Simba watashuka tena dimba la Uhuru kuwakaribisha Mashujaa FC Oktoba 13.

Baada ya kumalizana na mechi hizo za ligi ya ndani, nguvu zote za Mnyama zitahamishiwa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo watasaka tiketi ya kutinga Hatua ya Makundi.

Simba watacheza mchezo wa kwanza wa raundi ya pili ugenini kati ya Oktoba 16–18 dhidi ya FC 15 de Agosto (Equatorial Guinea) au Fomboni FC (Comoros) kabla ya kurejea Dar es Salaam kwa mchezo wa marudiano uliopangwa kufanyika kati ya Oktoba 23–25.

Kutokana na mchezo huo wa marudiano wa CAF kuangukia wikiendi ileile ya mchezo wa Mbeya City, Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) inatarajia kuweka kiporo mchezo huo ili kupisha mechi ya ligi ya mabingwa.

Mwezi huu utafungwa mkoani Arusha tarehe 28 Oktoba, pale Simba watakaposafiri kuwafuata Fountain Gate FC kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
1h ago
READ MORE β†’
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
5h ago
READ MORE β†’
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
19h ago
READ MORE β†’
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
23h ago
READ MORE β†’
Huyu Libasse ni moto kweli
Huyu Libasse ni moto kweli
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
2d ago
READ MORE β†’