Klabu ya Simba imethibitisha kuwa itacheza mechi mbili za kujipima nguvu Afrika Kusini kabla ya kurejea nchini.
Kulingana na ratiba iliyotolewa na Wekundu hao wa Msimbazi, mchezo wa kwanza utapigwa kesho Ijumaa Oktoba 02 dhidi ya Polokwane City.
Mechi ya pili itapigwa Jumamosi Oktoba 03 dhidi ya Sekhukhune United ukitarajiwa kupigwa katika mji wa Jonahanesburg.
Simba imeweka kambi ya siku 10 nchini Afrika Kusini ikiwa sehemu ya maandalizi yake wakati huu ambao ligi imesimama kupisha kalenda ya FIFA.

ADVERTISE HERE