Kikosi cha Simba leo kinaingia siku ya sita ya maandalizi yake Afrika Kusini kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Yanga utakaopigwa Oktoba 10 pamoja na mechi nyingine zitakazofuata baada ya mapumziko ya kalenda ya FIFA.
Kocha Mkuu wa Simba Steve Barker amepata muda wa kutosha kufanya maboresho muhimu ya kimbinu kwa kikosi chake wakati huu ambao ligi imesimama kupisha kalenda ya FIFA.
Mnyama ana jambo lake msimu huu, siku hizi 10 zinatumika ipasavyo kuiweka Simba katika mazingira bora zaidi ya kiushindani.










ADVERTISE HERE