Simba Queens yaifumua Yanga Princess 3-0 yatinga fainali Ngao ya Jamii

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
30 Sep 2026
Simba Queens yaifumua Yanga Princess 3-0 yatinga fainali Ngao ya Jamii

Timu ya Simba Queens imefuzu hatua ya fainali ya Ngao ya Jamii Wanawake 2026 baada ya kuichapa Yanga Princess mabao 3-0 katika mchezo wa nusu fainali.

Simba Queens ilitawala mchezo huo na kupata mabao yake kupitia Vivian Corazone, Senaf Wakuma na Merry Siyame, yaliyoiwezesha timu hiyo kupata ushindi mnono dhidi ya wapinzani wao wa jadi.

Kwa matokeo hayo, Simba Queens sasa itakutana na JKT Queens katika fainali ya Ngao ya Jamii Wanawake 2026.

JKT Queens ilitinga fainali baada ya kuifunga Mashujaa Queens bao 1-0 katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali.

Kwa upande mwingine, Yanga Princess na Mashujaa Queens zitakutana katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu wa mashindano hayo.

Simba Queens imeendeleza ubabe dhidi ya Yanga Princess wakigawa vipigo kwa watani zao hao kila timu hizo zinapokutana.

Ushndi huo umewapa bonus ya Tsh Milioni 20 wachezaji wa Simba Queens kutoka kwa mlezi wa timu hiyo Fatema Dewji

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
1h ago
READ MORE β†’
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
5h ago
READ MORE β†’
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
19h ago
READ MORE β†’
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
23h ago
READ MORE β†’
Huyu Libasse ni moto kweli
Huyu Libasse ni moto kweli
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
2d ago
READ MORE β†’