Simba Queens kazi ni moja leo dhidi ya Yanga Princess Ngao ya Jamii

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
30 Sep 2026
Simba Queens kazi ni moja leo dhidi ya Yanga Princess Ngao ya Jamii

Pazia la ligi kuu ya Wanawake linazinduliwa kwa mechi za Ngao ya Jamii ambapo leo mechi za nusu fainali zitapigwa uwanja wa KMC Complex.

Mabingwa watetezi Simba Queens wanatarajia kuchuana na watani zao wa jadi Yanga Princess katika mchezo utakaopigwa saa 12 jioni.

Mchezo huo utatanguliwa na mchezo wa kwanza wa nusu fainali kati ya JKT Queens dhidi ya Mashujaa Queens.

Baada ya kutofanya vyema kwenye michuano ya CECAFA na kukosa tiketi ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu, Simba Queens itashuka dimbani leo ikiwa na dhamira ya kumaliza hasira za kukosa tiketi ya ligi ya mabingwa na kufungua msimu mwingine na taji.

Kwa misimu ya karibuni Simba Queens imetawala dabi ya Kariakoo kwa upande wa Wanawake, bila shaka vijana wa kocha Mussa Mgosi leo wataendeleza ubabe wao dhidi ya wapinzani wao hao.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
1h ago
READ MORE β†’
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
5h ago
READ MORE β†’
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
19h ago
READ MORE β†’
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
23h ago
READ MORE β†’
Huyu Libasse ni moto kweli
Huyu Libasse ni moto kweli
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
2d ago
READ MORE β†’