Matola arejea Dar kuhudhuria kozi maalum ya CAF

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1 Oct 2026
Matola arejea Dar kuhudhuria kozi maalum ya CAF

Kocha Msaidizi wa Simba Suleiman Matola amerejea jijini Dar es salaam kuhudhuria kozi maalum inayotolewa na CAF kwa makocha wenye leseni A.

Matola alikuwa Afrika Kusini na kikosi cha Simba kilichoweka kambi maalum kwenye mji wa Polokwane kwa ajili ya maandalizi ya mechi zinazofuata baada ya mapumziko ya kalenda ya FIFA.

Matola amethiitisha kozi hiyo ni ya siku tatu ambayo imemfanya arejee jijini Dar es salaam huku akiwaacha wenzake kwenye benchi la ufundi wakiongozwa na kocha Steve Barker wakiendelea na kambi hiyo itakayodumu kwa siku 10.

“Narudi Dar es Salaam leo (jana) nina kozi fupi ya siku tatu ya Leseni A ya CAF ni utaratibu wa kawaida kwa makocha kusoma kila baada ya muda mfupi."

“Nitakuwa hapo kwa siku chache pamoja na makocha wengine mbalimbali kuhakikisha kuna kitu kipya napata,’’ Matola alinukuliwa na Mwanaspoti

Matola alikamilisha mafunzo yake ya ukocha mwaka jana na kupata leseni ya A ya CAF sasa akirejea kwa ajili ya 'refresher' kozi.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
1h ago
READ MORE β†’
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
5h ago
READ MORE β†’
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
19h ago
READ MORE β†’
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
23h ago
READ MORE β†’
Huyu Libasse ni moto kweli
Huyu Libasse ni moto kweli
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
2d ago
READ MORE β†’