Kikosi cha Simba Queens leo kinakamilisha maandalizi kuelekea mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya watani zao Yanga Princess.
Kesho Jumatano, Simba Queens wataumana na Yanga Princess katika mchezo utakaopigwa saa 12 jioni kwenye uwanja wa KMC Complex.
Pazia la msimu mpya wa ligi kuu ya Wanawake 2026/27 linazinduliwa kwa mechi hizo za Ngao ya Jamii.
Simba Queens ndio mabingwa watetezi wa ligi hiyo ambayo msimu uliopita walitwaa pasipo kupoteza mchezo wowote.
Kinadada hao wanaonolewa na Kocha Mussa Mgosi wamedhamiria kurejea msimu huu kwa nguvu kubwa wakitoka kupoteza nafasi ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa ya Wanawake msimu huu.
ADVERTISE HERE