TFF yajaza nafasi ya Katibu Mkuu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
28 Sep 2026
TFF yajaza nafasi ya Katibu Mkuu

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limejaza nafasi ya Katibu Mkuu kwa kumteua Evans Mgeusa, katika mabadiliko mapya ya uongozi yaliyofanywa na Kamati ya Utendaji ya shirikisho hilo.

Uamuzi huo umefikiwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya TFF kilichofanyika jijini Dar es Salaam chini ya Rais wa shirikisho hilo, Wallace Karia.

Mgeusa anachukua nafasi hiyo baada ya Oscar Mirambo, ambaye alikuwa akikaimu nafasi ya Katibu Mkuu, kuhamishiwa katika jukumu jingine ndani ya TFF.

Kabla ya uteuzi huo, Mgeusa alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Njombe (NIOREFA), na sasa anakabidhiwa jukumu la kusimamia shughuli za kiutendaji za sekretarieti ya TFF.

Katika mabadiliko hayo, Mirambo ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu, huku Mustapha Yusuph akiteuliwa kuwa Mkurugenzi mpya wa Fedha.

TFF pia imefanya mabadiliko katika baadhi ya nafasi za wakurugenzi, ambapo Kurugenzi ya Sheria, Habari na Masoko imegawanywa na kuwa kurugenzi tatu tofauti.

Hassan Njama ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Biashara na Masoko, Boniface Wambura akipewa nafasi ya Mkurugenzi wa Sheria, wakati Cliford Ndimbo ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
15 de Agosto yawasili Dar kwa mchezo dhidi ya Simba
1h ago
READ MORE β†’
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
15 de Agosto wanaandaliwa dozi saizi yao
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
5h ago
READ MORE β†’
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
CAF yabadili mwamuzi wa mchezo wa 15 de Agosto dhidi ya Simba SC
19h ago
READ MORE β†’
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
Wanasimba kushuhudia mchezo dhidi ya 15 de Agosto kwenye skrini kubwa Mwembeyanga
23h ago
READ MORE β†’
Huyu Libasse ni moto kweli
Huyu Libasse ni moto kweli
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
Mnyama amepania kumaliza mechi mapema Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
Mara Paap!, Dube anatua Msimbazi
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
Barker aweka mkakati wa kuwaadhibu 15 de Agosto licha ya kuwazuia mashabiki
2d ago
READ MORE β†’