Kiungo mshambuliaji wa Simba Clatous Chama 'Mwamba wa Lusaka' amewasili Polokwane Afrika Kusini kuungana na kikosu cha Wekundu hao wa Msimbazi ambacho kinaendelea na kambi maalum ya siku 10.
Chama ni miongoni mwa wachezaji waliochelewa kutua Afrika Kusini kutokana na changamoto za hati ya kuingia nchini humo.
Nyota wengine ni pamoja na Libasse Gueye na Anicet Oura ambao pia walitarajiwa kuwasili wakati wowote.
Chama ameungana na Ismail Toure, Elie Mpanzu, Rushine de Reuck, Ibrahim bajabeer, Neo Maema miongoni mwa nyota wa kigeni ambao tayari wako Polokwane wakiendelea na maandalizi.
Simba inatumia kambi hii kama sehemu ya maandalizi yake ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Yanga utakaopigwa Oktoba 10 pamoja na mechi nyingine za ligi kuu na ligi ya mabingwa.